WAWA, NYONI WAPEWA ONYO KALI

WAWA, NYONI WAPEWA ONYO KALI

5828
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM


KOCHA wa zamani Simba, Talib Hilal, amewataka mabeki wa timu hiyo kuwa makini na washambuliaji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Hilal amesema licha ya kwamba yupo nchini Oman, lakini anaifuatilia Ligi Kuu Tanzania Bara na kugundua Yanga wana safu nzuri ya ushambuliaji.

Akizungumza na BINGWA jana kwa njia ya mtandao, Talib alisema kutokana na hali hiyo, ni lazima safu ya ulinzi ya Simba inayoongozwa na Pascal Wawa na Erasto Nyoni kuwa makini.

“Timu yoyote ambayo inafunga mabao mengi ujue ina safu kali ya ushambuliaji, ndiyo maana nasema hawa mabeki wa Simba wanatakiwa kuwa macho muda wote wa dakika 90,” alisema Talib.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa msimu uliopita, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, kabla ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mzunguko wa pili, mechi  zilizochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

KUSHIRIKI
Makala ya awaliYANGA WATEGUA MITEGO
Makala ijayoMATOLA AMUOTA SALAMBA

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU