50 CENT AGEUKIA MASUMBWI

50 CENT AGEUKIA MASUMBWI

7161
0
KUSHIRIKI

NEW YORK, Marekani


 

STAA wa muziki wa hip hop, 50 Cent, ametajwa kuanza kujisogeza katika mchezo wa masumbwi ingawa haijafahamika kama atapanda ulingoni.

Bado haijawekwa wazi kama atakuwa mpiganaji au promota lakini amekuwa akionekana mara kadhaa akiwa na Rais wa Chama cha mchezo wa Ngumi na Mateke, Scott Coker.

Akisimulia alichozungumza na Cent, Coker alisema: “Nilimwambia mengi kuhusu mfumo wa kusajili mabondia na mengine mengi.

“Alivutiwa na aliniuliza maswali mengi na mazuri,” alisema Coker.

Siku chache zilizopita, Cent mwenyewe aliposti picha akiwa na mkongwe wa ngumi, Quinton ‘Rampage’ Jackson, hivyo kuibua tetesi kuwa huenda wakapanda ulingoni.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU