AGUERO ADAI ANAJIHISI KAMA KAZALIWA UPYA

AGUERO ADAI ANAJIHISI KAMA KAZALIWA UPYA

3272
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


 

STRAIKA wa Manchester City, Sergio Aguero, amesema kwamba anajisikia kama kazaliwa upya, baada ya kupona jeraha la upasuaji wa goti alilofanyiwa mwishoni mwa msimu uliopita.

Staa huyo wa timu ya Taifa ya Argentina, alifanyiwa upasuaji huo Aprili mwaka huu na jambo hilo likamfanya azikose mechi sita za mwisho.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, ameuanza msimu huu akiwa katika ubora wa hali ya juu na ndiye aliyefunga mabao mawili wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea kabla ya kutupia ‘hat-trick’ katika mechi ambayo waliondoka na ushindi wa mabao 6-1  dhidi ya Huddersfield Town katika michuano ya Ligi Kuu England.

Licha ya kushindwa kufunga mabao katika mechi nyingine tatu za ligi,  Aguero alisema juzi kwamba ndio kwanza ameonja ladha ya kucheza bila maumivu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita.

“Kwa kuwa mkweli najisikia ni wa ajabu,” staa huyo alikaririwa na tovuti ya klabu akisema.

“Dk. Cugat alinifanyia kazi kubwa katika goti langu na wala sijisikii matatizo yoyote,” aliongeza straika huyo.

“Wakati wa kipindi cha miaka michache iliyopita nilikuwa nikisikia maumivu na ilipofika mwishoni mwa msimu uliopita ndio tukaamua ni muda mwafaka kuanza matibabu na matokeo yake yamekuwa mazuri,” alikwenda mbali zaidi staa huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU