AMRI SAID ALA MAISHA MBAO FC

AMRI SAID ALA MAISHA MBAO FC

7333
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI


KOCHA wa Lipuli FC, Amri Said, amesaini mkataba wa mwaka mmoja  kuifundisha Mbao FC kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Said amechukua mikoba ya kocha  Mrundi, Ettiene Ndayiragije, aliyejiunga na KMC iliyopanda daraja katika msimu uliopita wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi, alisema waliingia mkataba huo na Said jana jijini Dar es Salaam, baada ya kuridhishwa na utendaji wake wa kazi akiwa Lipuli.

Njashi alisema wameamua kumchukua kocha huyo kutokana na kiwango  kilichoonyeshwa na Lipuli katika msimu uliopita, hivyo anaamini ataendeleza makali hayo akiwa  na timu yao ya Mbao FC.

“Amri Said ni mmoja wa makocha  bora ndiyo sababu tumeamua kumchukua yeye na si mwingine, tunaamini ataisaidia Mbao FC kufika mbali, umeona alichokifanya Lipuli,” alisema Njashi.

Baada ya Ndayiragije kuondoka, timu hiyo ya Mbao ilikuwa chini ya Novatus Fulgence.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU