ANS AREMEYAW ANAVYOWAUMBUA WALARUSHWA SOKA AFRIKA

ANS AREMEYAW ANAVYOWAUMBUA WALARUSHWA SOKA AFRIKA

8412
0
KUSHIRIKI

ACCRA,Ghana

HABARI za uchunguzi ni moja ya eneo ambalo waandishi wengi wa habari wamekuwa wakijichukulia sifa kubwa, baada ya kuweka adharani uozo ambao umeghubika katika sekta mbalimbali duniani.

Na moja ya uchunguzi huo  ni ambao umewekwa adharani  wiki hii katika soka la Afrika na kuacha maswali mengi likiwamo pengine ndio maana soka  la baadhi ya nchi katika  bara hili kushindwa kupiga hatua.

Katika uchunguzi huo,uliofanywa na mwandishi wa habari mahiri nchini Ghana, Anas Aremayaw Anas, ulifanikisha kuwanasa maofisa  zaidi ya 100 kutoka mashirikisho ya soka Afrika  akiwamo Rais wa Shirikisho la Soka Ghana, GFA, Kwesi Nyantakyi na kusababisha serikali ya nchi hiyo kuingilia kati na kulivunja.

Ghana ilifikia hatua hiyo ambayo ilitangazwa na Waziri wa Habari ,  Mustapha Abdul-Hamid,, baada ya  Nyantakyi  kupigwa  picha akipokea dola 65,000 kutoka kwa mwandishi habari huyo mpekuzi aliyejifanya kuwa mfanyibiashara ambaye anataka kuwekeza katika soka katika soka Ghana.

Katika makala hiyo ndefu ya video, iliyopewa jina ‘wakati ulafi na rushwa zinapokuwa kawaida’, ambayo ilinaswa na   Kitengo cha upekuzi cha Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kiitwacho, Africa Eye,  ilikabidhiwa kwa maofisa wa serikali mwezi uliopita na kuonyeshwa wazi mbele ya umma kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.

Nyantakyi ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka  Afrika (CAF) na pia NI Mjumbe  wa Baraza la Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA,  taasisi inayosimamia soka duniani ambaye tangu  achukuwe uongozi wa  GFA, wito wake ulikuwa ni kusimamia mapambano  dhidi ya  rushwa.

Hata hivyo katika makala hiyo ya upekuzi inamuonyesha akiweka pesa hizo  dola 65,000  ambazo zinadaiwa zilikuwa ni kwa ajili ya kununua vifaa vya michezo akiziweka kwenye mfuko mweusi wa plastiki kwa hapa nchini ‘Rambo’.

*Picha kamili ilivyokuwa

Taarifa zinaeleza kwamba  ili kuhakikisha mambo yao yanakwenda sawia, kikosi cha mzalishaji filamu hiyo, walimuita Nyantakyi  katika hoteli ya kifahari  iliyopo katika moja ya nchi za Mashariki  ya Kati  kwa ahadi kuwa atakutana na mfanyabiashara tajiri  mwenye hamu ya  kuingia  mkataba wa uwekezaji na GFA.

Zinaeleza, baada ya kupata mwaliko huo na bila kufahamu kama yupo mtegoni ,Nyantakyi alifunga safari  hadi alikoelekezwa na wenyeji wake na baada ya kupolewa ndipo ukaaanza mchakato wa majadiliano ya kuingia mkataba.

Baada ya majadiliano hayo, Nyantakyi alijadiliana na kuandika mkataba huo wa ufadhili kwa niaba ya Chama Cha Soka Ghana ambao  moja ya kipengele ungeruhusu sehemu ya ufadhili huo kuelekezwa katika kampuni anayoimiliki.

Inaelezwa kwamba kama ndili hilo lingekuwa la kweli kusingekuwapo na chochote kwani mzigo wote ungeishia kwenye miradi yake.

Hatua hii ni sehemu ya uchunguzi wa miaka miwili uliofanywa na mwandishi huyo, Aremeyaw na ambao umefanikiwa kuwaumbua maofisa mbalimbali Afrika ambao wanajihusisha na vitendo hivyo vya rushwa.

Miongoni mwa waliotumbukia kwenye mtego huo ni mwamuzi  wa soka  kutoka Kenya, Aden Range Marwa, ambaye alitarajiwa kusimamia mechi za Kombe la Dunia nchini Urusi.

Katika  mtego wa mwandishi huyo, mwamuzi huyo msaidizi  alikubali dola 600 kutoka kwa mtu aliyejifanya kuwa ofisa wa Shirikisho la Soka la Ghana, wakati wa mechi za fainali za Mataifa ya Afrika mwaka jana ili aweze kupanga matokeo.

Katika picha hiyo ya video, Marwa  anaonekana akipokea mzigo huo kutoka kwa mwandishi huyo ambaye alikuwa amejifunika sura na huku akishukuru kwa zawadi hiyo, lakini akamtaka wafahamiane.

“Ufahamu nashukuru kwa zawadi hii, lakini jambo la muhimu katika urafiki wetu ni kila mmoja kumfahamu mwenzake,” Marwa anasikika akisema katika video hiyo mara baada ya kuchukua kiasi hicho cha fedha kabla ya mechi kuanza.

Kwa kashifa hiyo tayari FIFA imeshatangaza  kibarua chake kimeshatumbukia nyongo na hivyo hatakwenda tena Urusi, ingawa mwenyewe anakanusha tuhuma hizo ambapo mwalimu huyo ambaye ni mtaalmu wa masomao ya Hisbati na Kemia  katika shule ya Sekondari ya  Komotobo iliyopo Wilaya ya  Migori  atakuwa amepoteza kitacha Sh, milioni 2.5 za Kenya ambazo angezipokea kwa kila mchezo ambayo aneisimamia.

 * Aremeyaw Anas ni nani?

Anas Aremeyaw Anas  ni mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Ghana ambaye alialiwa mwishoni mwa miaka ya 1970s.

[1] Anas motto ambaye anajiita  “kina,aibu na jela ni maarufu kwa kutumia kalamu yake  katika habri za uchunguzi  na hakuna mtu ambaye alikuwa akifahamu sura  yake hadi alipoionesha wakati wa mahojiano na Shirika la  Utangazji la Uingereza  BBC , Novemba  2015 wakati akihojiwa.

Tofauti na waandishi wengine wa vyombo vya habari ambao wamejikita katika kunadaa vipindi na  kuandika makala,  Anas  yeye ameelekeza nguvu zake katika habari za kutetea haki za binadamu na mapambano dhidi ya  rushwa nchini Ghana na katika nchi za Ukanda wa Sahara.

 

Kwa umahiri wake, mwandishi huyo wa habari aliwahi kusifiwa na aliyekuwa Rais Marekani Barack Obama alipofanya ziara nchini humo kwa kuhatarisha maisha yake  ili kueleza ukweli.

Mpaka sasa Anas ameshashinda zaidi ya tuzo  17 za kimataifa kwa kazi yake ya uchunguzi  na  mwaka 2011 alishika  nafasi ya tano kwawatu wenye ushawishi nchini waliotajwa na Kituo cha Televisheni cha e.tv Ghana na kisha Desemba 2014 akatangazwa mshindi wa tuzo ya mwaka kwa  mtu mwenye ushawishi Afrika iliyotolewa na jarida la  New African.

Mbali na tuzo hiyo na nyinginezo, Desemba  2015  jarida la Foreign Policy, lilimtaja  Anas  kuwa mmoja watu wenye kikra duniani ambazo zimewahi kunyakuliwa na watu mahiri kama vile  Barack Obama, Aung San Suu Kyi, Pope Benedict XVI na  Malala Yousafzai.

Hizo ni baadhi tu ya sifa alizonazo mwandishi huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU