BRAZIL, UJERUMANI ZITAKAVYOTAMBA KWA MKWANJA KOMBE LA DUNIA

BRAZIL, UJERUMANI ZITAKAVYOTAMBA KWA MKWANJA KOMBE LA DUNIA

5078
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


 

FAINALI za Kombe la Dunia ziko njiani. Ni vita ya mwezi mmoja itakayoyakutanisha mataifa 32 itakayoanza mwezi ujao, Juni 14 na kufikia tamati Julai 15.

Hata hivyo, kati ya hizo 32, kuna timu 10 zitakazokuwa zikibamba kwa vikosi vyake kuwa na mastaa wa bei kali.

Mtandao wa Transfermarket umeifanya kazi hiyo na kugundua kuwa ni Brazil ndiyo itakayokuwa na kikosi cha bei mbaya zaidi.

Timu hiyo inayofahamika kwa jina la utani la ‘Selecao’ (wateule), kitakuwa na mastaa wenye thamani ya euro milioni 673 (zaidi ya Sh tril 1.8 za Tanzania).

Wakali hao wa Samba wanatambia kikosi chao ambacho sehemu kubwa ya wachezaji wake (asilimia 88) wanakipiga nje ya Brazil, wengi waking’ara barani Ulaya. Neymar pekee ana thamani ya euro milioni 150.

Nafasi ya pili inakamatwa na Ujerumani ambao wanatarajiwa kwenda Urusi wakiwa na kikosi chenye thamani ya euro milioni 636.

Hiyo ni kwa kuwa zaidi ya asilimia 40 ya mastaa wake ni wale wanaocheza katika mataifa mengine. Ukimtazama Leroy Sane pekee anayecheza Manchester City, ana thamani ya euro milioni 50.

Timu ya Taifa ya Ufaransa inafuata kwani kikosi chake kinachotarajiwa kuwa Urusi kwa mwezi mmoja kinatajwa kuwa na thamani ya euro milioni 636.

Mtandao wa Transfermarket umeonesha kuwa asilimia 58 ya mastaa watakaokuwa na kikosi hicho nchini Urusi, wanakipiga nje ya Ufaransa.

Mchezaji wao ghali zaidi ni kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, ambaye kumng’oa Old Trafford utalazimika kuandaa si chini ya euro milioni 110.

Wahispania wanakamata nafasi ya nne kwani wao wana kikosi kinachogharimu euro milioni 603. Asilimia 42 ya wachezaji wake wanakipiga nje ya La Liga (Ligi Kuu ya Hispania).

Morata mwenye thamani ya euro milioni 30 ndiye mchezaji wa bei kali katika kikosi kinachotarajiwa kukwea pipa na kwenda kuiwakilisha Hispania nchini Urusi.

Nafasi ya tano inakamatwa na Argentina yenye kikosi cha euro milioni 529 na asilimia 85 ya mastaa wake wanacheza nje.

Mbali ya mchango wake wa mabao na ‘asisti’ pindi fainali hizo zitakapoanza, Lionel Messi ndiye mchezaji ghali pia kikosini, akiwa na thamani ya euro milioni 131.

Ubelgiji wanafuata kwa kikosi chao cha euro milioni 504, huku wachezaji wake wengi (asilimia 92) wakiwa wanacheza Ulaya. Staa ghali kwao ni mkali wa Chelsea, Eden Hazard na sokoni anapatikana kwa euro milioni 75.

Waingereza wanakatamata nafasi ya saba kwani kikosi chao kinagharimu euro milioni 339 na ni asilimia 4 pekee ya mastaa wanaocheza nje ya Ligi Kuu England (EPL).

Croatia nao wamo, wakiwa nyuma ya England kwa kikosi chao cha euro milioni 295. Mastaa wengi (asilimia 87) watakaokuwa na timu hiyo Urusi ni wale wanaotamba Ulaya, akiwamo Luca Modric wa Real Madrid.

Wareno watakaokuwa wakiongozwa na nahodha wao, Cristiano Ronaldo, wako nafasi ya tisa kwa kuwa na kikosi cha bei kali (euro milioni 279).

Huku asilimia 70 ya wanasoka wake wakiwa nje ya Ureno, Ronaldo ndiye ghali zaidi, kwani bei yake sokoni si chini ya euro milioni 130.

Poland ya Roberto Lewandowski inafunga dimba katika timu 10 zitakazokuwa na mastaa wa bei kali katika fainali za mwaka huu, wakiwa na bei thamani ya euro milioni 220.

Pia, watakwenda Urusi wakiwa na kikosi chenye asilimia 64 ya wachezaji wanaocheza nje ya taifa hilo ambalo sehemu kubwa ya wakazi wake ni waumini wa Dini ya Kikiristo (zaidi ya asilimia 87).

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU