BRITNEY SPEARS AGEUKA KITUKO JUKWAANI

BRITNEY SPEARS AGEUKA KITUKO JUKWAANI

5461
0
KUSHIRIKI

 LONDON, England


 

MWANAMUZIKI mkongwe, Britney Spears, amegeuka kituko jukwaani baada ya kusahau anakotumbuiza na hivyo kulazimika kuomba msaada kwa wanenguaji wake.

Tukio hilo limetokea juzi wakati Malkia huyo wa miondoko ya Pop, akitumbuiza katika tamasha la Brighton Pride lilofanyika katika viwanja vya Preston Park, nchini Uingereza, ikiwa ni baada ya kuondoka nchini Marekani ili akaendelee na ziara yake nchini humo.

Hata hivyo, wakati akiwa katikati mwa tamasha hilo, staa huyo aliamua kuwafuata wanenguaji wake na kuwauliza hapo ni mahali gani walipo, ndipo wakamweleza kuwa wapo katika mji huo wa Brighton Pride na baada ya kuambiwa hivyo, mkongwe huyo ndipo akaanza kupaza sauti akiwasalimia mashabiki wa mji huo.

Kituko hicho kilionekana kusambaa kwa haraka katika mitandao ya kijamii ukiwamo wa Twitter, lakini mashabiki wengi walionekana kutokitilia maanani na badala yake wakamtetea mwimbaji huyo wa kibao cha Toxic.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU