CARRAGHER ‘AMVAMIA’ MMILIKI WA LIVERPOOL

CARRAGHER ‘AMVAMIA’ MMILIKI WA LIVERPOOL

691
0
KUSHIRIKI

MERSEYSIDE, Liverpool

MMILIKI wa klabu ya Liverpool, John Henry, ameanza kuonja joto ya jiwe kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo waliochukizwa na kutoona mchezaji yeyote akisajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili la Januari.

Bosi huyo wa Kimarekani aliwakera zaidi wanazi wa Liver pale walipoona ‘tweet’ yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ikihusu mchezo wa Super Bowl unaochezwa nchini Marekani, ambapo malalamiko ya mashabiki wengi wa Liverpool hayakutokana tu na hasira za kutoona mchezaji mpya bali pia yalihusisha na kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Hull City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Naye mchambuzi wa soka wa SkySport, Jamie Carragher, ambaye aliwahi kukipiga Liverpool, alisema kinachoiangusha timu hiyo kwa sasa ni kutokuwa na kikosi kipana ambacho kingeiwezesha kuchuana vilivyo kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

“Ni jambo la kusikitisha kuona hakuna nyongeza ya wachezaji iliyofanyika Januari. Sisemi ufanyike usajili wa kukurupuka, hapana, wachezaji wa kusajili mbona walikuwapo sokoni!

“Ila ninachokisisitiza ni kwamba, Liverpool ilihitaji kuwa na idadi fulani ya wachezaji. Ukilitazama benchi lao, halina nguvu kama benchi la Manchester United lilivyo.

“Unafahamu kwanini wameporomoka kutoka kuwa tishio la ubingwa kwa Chelsea? Ni kwa sababu hawana kikosi kipana cha kupambana na wengine,” alisema Carragher.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU