CONTE AIITA MEZANI CHELSEA

CONTE AIITA MEZANI CHELSEA

8145
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


 

ANTONIO Conte amesisitiza kuwa kwa sasa anaendelea kufanya kazi kulingana na mkataba wake katika klabu ya Chelsea, lakini anahisi neno la mwisho kuhusu hatima yake linatakiwa kutoka kwa mabosi, akionekana kuhitaji kikao cha mazungumzo.

Licha ya kuipa timu hiyo taji la Ligi Kuu England msimu uliopita ambao ulikuwa ni wa kwanza kwa Muitaliano huyo, tetesi ziliibuka kuwa kocha huyo hafurahishwi na sera ya usajili ya Chelsea na huenda akatimka.

Sekeseke hilo lilianzisha tetesi nyingine zilizowahusisha kocha wa Napoli, Maurizio Sarri na Massimiliano Allegri wa Juventus, mmojawapo huenda akarithi mikoba ya Conte msimu ujao.

“Ninachojua kuwa kwa sasa mimi ni kocha wa Chelsea. Ni ngumu kuzungumzia tetesi kwa sasa, nafahamu zipo tangu msimu huu ulipoanza, kimsingi hazina umuhimu kwangu,” alisema Conte.

“Ili uamuzi wa hatima yangu ufikiwe, inabidi pande mbili zikutane. Siwezi kujiamulia tu. Klabu ipo, kuna watu wa kuamua mambo yaende vipi, sifanyi kazi peke yangu,” aliongeza kocha huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU