DRAKE, MEEK MILL HAKUNA TENA ‘JINI KISIRANI’

DRAKE, MEEK MILL HAKUNA TENA ‘JINI KISIRANI’

5118
0
KUSHIRIKI

BOSTON, Marekani


ULE ugomvi wa muda mrefu kati ya marapa, Drake na Meek Mill, umezikwa bwana na sasa mastaa hao ni maswahiba wakubwa katika soko la muziki.

Bifu lao lilizikwa rasmi usiku wa Ijumaa ya wiki iliyopita, ambapo Drake akiwa jukwaani katika Ukumbi wa TD Garden alimwita jukwaani msanii mwenzake huyo.

Baada ya Meek kupanda jukwaani, alianza kupeana mkono na Drake, huku kila mmoja akiachia tabasamu, jambo lililoonesha kuwa hakuna tena ‘jini kisirani’ kati yao.

Haikuishia hapo, wasanii hao walishirikiana mwanzo mwisho kuuimba wimbo wa Meek uitwao ‘Dreams &Nightmares’ ambao ulitikisa mwaka 2012.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU