DUA LIPA KUTUMBUIZA FAINALI UEFA

DUA LIPA KUTUMBUIZA FAINALI UEFA

8261
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


 

STAA wa muziki wa Pop kutoka England, Dua Lipa, anatarajiwa kupiga shoo katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu itakayochezwa jijini Kiev, Ukraine baina ya Real Madrid na Liverpool.

Mei 26, mwaka huu ndiyo tarehe rasmi ya fainali hiyo ambayo itachezwa kwenye Dimba la NSC Olimpiyskiy.

Dua Lipa anayetamba na ngoma yake maarufu kwa sasa ya ‘New Rules’, atatumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka duniani.

“Nilifurahi mno nilipoombwa na UEFA pamoja na wadhamini wa mashindano, Pepsi, kwa ajili ya kutumbuiza katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hii ni fursa inayokuja mara moja tu kwenye maisha,” alisema mwanadada huyo.

“Nasubiri kwa hamu nitakapoimba mbele ya mashabiki na kushiriki tukio muhimu la mtanange wa soka. Najipanga kufanya shoo kali itakayokumbukwa,” aliongeza mkali huyo ambaye atafuata nyayo za The Black Eyed Peas na Alicia Keys waliowahi kutumbuiza kwenye fainali zilizopita.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU