FABREGAS ‘AWACHANA’ MASTRAIKA CHELSEA

FABREGAS ‘AWACHANA’ MASTRAIKA CHELSEA

5391
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


 

KIUNGO wa klabu ya Chelsea, Cesc Fabregas, amewalaumu washambuliaji wa timu yake hiyo kwa kukosa nafasi nyingi za kufunga mabao msimu huu.

Kiungo huyo alitarajiwa kuitumikia timu yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa kuamkia leo dhidi ya Huddersfield.

Chelsea imekuwa na kiwango cha kuridhisha hivi sasa katika harakati zao za kutaka kumaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, ingawa imekumbwa na tatizo la kutofunga mabao ya kutosha.

Tangu Februari mwaka huu, ‘The Blues’ hao wameweza kufunga zaidi ya mabao mawili katika mechi moja tu, wakipata zaidi sare za bila kufungana katika mechi saba za mwezi Desemba na Januari.

Fabregas anaamini ubutu wa washambuliaji ndio uliosababisha Chelsea ikose pointi za kutosha katika msimu huu.

“Tunapata nafasi za kutosha za kufunga kutokana na kujituma kwetu, lakini udhaifu wetu mkubwa ni kutofunga mabao,” alisema kiungo huyo.

“Nimeshuhudia nafasi nyingi zinazopatikana msimu huu zikishindwa kutumika vyema na washambuliaji wetu, hizo nafasi zingetuwezesha kushinda mechi ambazo hatukuweza kuibuka na ushindi,” aliongeza.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU