GUARDIOLA AMKATAA STERLING

GUARDIOLA AMKATAA STERLING

5277
0
KUSHIRIKI

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema nyota wake, Raheem Sterling, si miongoni mwa wanasoka bora kwa sasa.

Hata hivyo, Guardiola aliongeza kuwa hilo linaweza kutokea hapo baadaye kwa kuwa bado ni mchezaji mwenye umri mdogo.

“Raheem ni mchezaji wa kiwango cha juu lakini ni mdogo mno kusema ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani,” alisema.

Sterling (23), alizipasia nyavu mara mbili katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Southampton katika mchezo uliochezwa juzi katika Uwanja wa Etihad.

Aidha, alihusika katika upatikanaji wa mengine mawili kwa kutoa pasi za mwisho ‘asisti’.

KUSHIRIKI
Makala ya awaliHAKATWI MTU
Makala ijayoBARUA YA MANJI YATULIZA ZOGO

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU