HABARI NJEMA YANGA

HABARI NJEMA YANGA

7708
0
KUSHIRIKI

CLARA ALPHONCE NA HUSSEIN OMAR


WAPENZI wa Yanga wametakiwa kutokuwa na presha kuelekea msimu ujao, kwani kwa mikakati iliyosukwa, timu yao itakuwa ni moto wa kuotea mbali Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, wamejikuta wakiporwa taji lao hilo walilolishikilia kwa misimu mitatu mfululizo na watani wao wa jadi, Simba.

Mbali ya kupokwa kombe la Bara, pia Yanga imeshindwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, baada ya kushindwa kufanya vema Kombe la Shirikisho Tanzania (Azam Sports Federation Cup), kipute ambacho kingewawezesha kupata tiketi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa kufahamu hilo, viongozi wa Yanga wakishirikiana na benchi la ufundi, wamekuwa wakiumiza vichwa kuona ni vipi wanarejesha makali ya kikosi chao msimu ujao.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, alisema kuwa, kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, yeye……..

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA hapo juu

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU