HAMISA MOBETTO AENDELEA KUPETA MAREKANI

HAMISA MOBETTO AENDELEA KUPETA MAREKANI

4973
0
KUSHIRIKI

WASHNGTON, MAREKANI

MWANAMITINDO ambaye amehamishia nguvu zake katika muziki, Hamisa Mobetto, ameendelea na ziara yake katika miji mbalimbali nchini Marekani akiongozana na Christian Bella.

Akizungumza na Papaso la Burudani, mwandaaji wa ziara hiyo, DMK Global, alisema onyesho la Mobetto na Christian Bella walilofanya Houston, Texas mwishoni mwa wiki iliyopita, lilikuwa kubwa na leo wanatarajia kukonga nyoyo za Watanzania wanaoishi katika mji wa Dallas.

“Ziara inaendelea vizuri, kesho (leo) tuna shoo nyingine Dallas ambayo nadhani itakuwa kubwa kuliko ile ya kwanza,” alisema DMK Global.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU