HENRY HUKO MONACO ANALIPWA BIL 17/-

HENRY HUKO MONACO ANALIPWA BIL 17/-

4314
0
KUSHIRIKI

MONACO, Ufaransa

HUENDA Thierry Henry ana sababu nyingi za kukifurahia kibarua chake kipya pale Monaco, lakini kubwa zaidi ni mshahara mnono anaolipwa na mabosi wa timu yake hiyo ya zamani.

Mfaransa huyo aliyewahi kutamba barani Ulaya akiwa na klabu za Arsenal na Barcelona, anakinga Pauni milioni 6 (zaidi ya Sh bil 17 za Tanzania) kwa mwaka.

Kiasi hicho cha fedha hakitofautiani na alichokuwa akilipwa kocha aliyempisha kiti cha kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo, Leonardo Jardim.

Ikizingatiwa kuwa Henry hana uzoefu mkubwa katika kazi ya ukocha, mkwanja huo kwake si haba.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU