ISHA MASHAUZI ASISITIZA MAADILI KWA WANAWAKE

ISHA MASHAUZI ASISITIZA MAADILI KWA WANAWAKE

4251
0
KUSHIRIKI

NA JEREMIA ERNEST


 

MSANII nyota wa Taarabu nchini, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, amewataka wanawake kuishi katika maadili na tamaduni  za Kiafrika kwa sababu ni walimu wa watoto katika jamii.

Mashauzi anayefanya vizuri na wimbo wa Sudi Sudini, ameliambia Papaso la Burudani kwamba mwanamke ni mwalimu wa mtoto hivyo anapofanya matendo machafu, husababisha madhara kwa jamii.

“Watoto wanaishi muda mwingi na wanawake, anaweza kuwa mama  au dada wa kazi, tunapokuwa majumbani tujaribu kulinda maadili ili mtoto akue katika maadili mema, watoto ni wepesi kuiga tunapotumia lugha mbaya kuwakanya ama kwenye maongezi wanakariri harafu baadaye wanayatumia,” alisema Mashauzi.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU