KAGERA SUGAR KUTIBUA UBINGWA WA SIMBA

KAGERA SUGAR KUTIBUA UBINGWA WA SIMBA

5772
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

BENCHI la ufundi la Kagera Sugar, limesema litahakikisha linapanga silaha zake kwa ukamilifu ili waweze kupata pointi tatu kutoka kwa Simba, katika mchezo wao utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kagera itakutana na Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, siku ambayo Wanamsimbazi hao watakabidhiwa kombe lao la ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Akizungumza na BINGWA wakiwa Kahama mkoani Shinyanga safarini kuja Dar es Salaam, Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alisema anafahamu Simba inahitaji kuweka rekodi ya kumaliza ligi wakiwa hawajafungwa kitu ambacho hawatafanikiwa.

“Wao wanataka kumaliza ligi wakiwa hawajafungwa, lakini sisi tunahitaji pointi tatu ili kujiwekea mazingira ya kuhakikisha tunasalia katika ligi kuu msimu ujao, hivyo ni vigumu kuwaacha watufunge kirahisi.

“Ukiangalia katika msimamo wa Ligi Kuu hadi sasa kuanzia timu inayoshika nafasi ya 11 ambayo ipo chini yangu, hadi ile inayoburuza mkia ni alama nane pekee nilizowazidi kama nikiruhusu kufungwa mechi zilizobaki nitakuwa katika hatari,” alisema.

Mexime aliongeza kuwa wanakuja jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha wanapata pointi tatu kutoka kwa Simba, ambazo zitawahakikishia kubaki katika ligi msimu ujao.

Msimamo wa ligi unaonyesha Kagera imecheza mechi 28, pointi 31 ikiwa nafasi ya 10, huku ikisaliwa na michezo miwili pekee dhidi ya Simba pamoja na Lipuli FC.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU