KILIFEST YAACHA GUMZO DAR

KILIFEST YAACHA GUMZO DAR

722
0
KUSHIRIKI

WASANII mbalimbali mwishoni mwa wiki hii waliacha historia kwenye tamasha la Kilifest lililofanyika kwa mara ya kwanza katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni Dar es Salaam. Tamasha hilo lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, lilikuwa la kuvutia baada ya mchanganyiko wa burudani
mbalimbali ikisimamiwa na MaDJ wazoefu kama DJ Summer, DJ Zero na DJ Mafuvu. Mbali na burudani hiyo wasanii mbalimbali waliweza kutumbuiza kwenye tamasha hilo lililojaza mashabiki mbalimbali. Wasanii waliotoa burudani ni Isha Mashauzi ambaye alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa vibao vyake na staili yake ya aina
yake ya uimbaji. Wengine waliotumbuiza ni pamoja na Mapacha Watatu, Maua, Ruby, Damian Soul, Navy Kenzo, Fid Q, Ben Paul, Vanessa Mdee, Shettah na Weusi ambao walifanya shoo ya aina yake na kuwafanya mashabiki wacheze na kuimba muda wote huku wakiwa na furaha. Akizungumza mara baada ya kumalizika tamasha hilo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, PamelaKikuli, aliwashukuru Watanzania kwa kuitikia vizuri na kujitokeza kwa wingi katika tamasha hili huku wakiahidi kuliboresha zaidi miaka inayokuja. “Tulidhamiria kufanya kitu kizuri na kwa kweli tumefurahishwa na jinsi watu wamepokea tamasha hili ambalo tuna nia ya kuliendeleza miaka ijayo ili kuweza kuwapa wateja wetu na wapenzi wa burudani kitu tofauti na cha aina yake.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU