LUKAKU KUCHEZA FAINALI KOMBE LA FA

LUKAKU KUCHEZA FAINALI KOMBE LA FA

7832
0
KUSHIRIKI

MANCHESTER, England


 

HUENDA straika wa Man United, Romelu Lukaku, akarudi mazoezini wiki hii katika harakati za kujiweka fiti kabla ya kuivaa Chelsea kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA.

Mfungaji bora huyo wa United msimu huu alikuwa nchini Ubelgiji chini ya uangalizi wa daktari maalumu, Lieven Maesschalck, akitibiwa jeraha la enka alilokumbana nalo katika mtanange wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal.

Lukaku mwenye umri wa miaka 24, anategemewa kurudi England leo. United itamfanyia vipimo zaidi katika makao makuu ya uwanja wao wa mazoezi, Carrington, kabla ya kurudi mazoezini kesho, siku chache kabla ya kushiriki fainali.

Huenda mshambuliaji huyo angecheza kwenye mechi ya mwisho ya ligi jana dhidi ya Watford, lakini aliepuka kutohatarisha hali yake kuelekea fainali za Kombe la Dunia mapema mwezi ujao.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU