LULU DIVA KUFANYA ZIARA LORD BADEN

LULU DIVA KUFANYA ZIARA LORD BADEN

4539
0
KUSHIRIKI

NA MEMORISE RICHARD

STAA wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, Jumamosi wiki hii anatarajia kufanya ziara yake katika shule ya Lord Baden iliyopo Bagamoyo, Pwani, kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi kuhusu mambo mbalimbali.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Lulu Diva alisema lengo la ziara hiyo ni kuzungumza na wanafunzi kuhusu kusoma kwa bidii pamoja na kuwasisitiza kusimamia ndoto walizojiwekea.

“Nikiwa kama msanii na kioo cha jamii, nina wajibu wa kuhakikisha natoa elimu kwa wanafunzi kuhusu kusoma kwa bidii na kuwahimiza kuishi katika ndoto zao na kuweka juhudi kwenye masomo, pia nitawapelekea zawadi na kuwaburudisha,” alisema Lulu Diva anayefanya vizuri na wimbo wa Homa.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo, Kanali Mstaafu Kipingu, aliongeza kuwa wamejiandaa kumpokea Lulu Diva na kuifanya ziara hiyo iwe maalumu kwa burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU