MAN FONGO AMRITHISHA MWANAWE SINGELI

MAN FONGO AMRITHISHA MWANAWE SINGELI

6125
0
KUSHIRIKI

NA KYALAA SEHEYE

NYOTA wa muziki wa singeli nchini, Aman Hamis ‘Man Fongo’, amesema ameanza kumwandaa mtoto wake wa kiume kuwa msanii mkubwa zaidi yake.

Man Fongo ameliambia Papaso la Burudani kuwa, amefurahi kupata mtoto wa kiume na anaomba sana arithi kazi yake ya kuimba singeli kama atahitaji.

“Nataka mtoto wangu aje kuwa msanii mkubwa kuzidi mimi na nimejipanga kumwandalia njia   ambazo zitakuwa rahisi yeye kufanikiwa kwa urahisi, kuliko njia ngumu nilizopitia, nitampatia elimu bora na kumfunza heshima na nidhamu ya hali ya juu,” alisema Man Fongo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU