MENEJA WA DIAMOND KUWASIMAMIA NAVY KENZO

MENEJA WA DIAMOND KUWASIMAMIA NAVY KENZO

8067
0
KUSHIRIKI

NA JEREMIA ERNEST


 

KUNDI la muziki wa Bongo Fleva, Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika, limeungana na Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ambwene Yessayah ‘AY’, kusimamiwa na meneja biashara, Sallam Sk.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Sallam Sk alisema kuanzia video ya wimbo mpya kutoka kwa kundi hilo, itaanza kusimamiwa na yeye na tayari amejipanga kulisimamia kundi hilo ili kulipa mafanikio zaidi.

“Mpaka sasa namiliki wasanii wakubwa wawili, AY na Diamond na sasa nitaanza kufanya kazi na Navykenzo, tayari wamenipa video tano nichague moja ya kuanza nayo,” alisema Sallam Sk katika hafla ya kuzaliwa kwake iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU