MKUDE: MIMI NI ZAIDI YA OKWI

MKUDE: MIMI NI ZAIDI YA OKWI

8427
0
KUSHIRIKI

NA SALMA MPELI


 

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, amesema hawezi kuondoka kwenye kikosi cha timu hiyo kwa sasa kwani ameitumikia kwa kipindi kirefu, akifanya hivyo wakati wa shida na raha, tofauti na wenzake aliokuwa nao mwanzo kama Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto.

Mkude ni miongoi mwa wachezaji hao watatu ambao walikuwapo katika kikosi kilichotwaa ubingwa kwa mara ya mwisho msimu wa 2011/12 kabla ya kuusotea kwa miaka mitano bila mafanikio hadi walipobeba ‘mwali’ msimu huu.

Kati ya watatu hao, ni Mkude pekee aliyedumu na Simba kwa wakati wote huo, huku wenzake hao wawili wakiondoka Msimbazi kwa nyakati tofauti kabla ya kurejea kundini.

Akizungumza na BINGWA baada ya mchezo wao dhidi ya Singida United walioibuka na ushindi wa bao 1-0 mjini Singida, Jumamosi iliyopita, Mkude alisema: “Siondoki Simba, nimekuwepo muda mrefu, nimeitumikia kwa shida na raha tangu tulipopata ubingwa wetu wa mwisho 2011/12 hadi leo, wakati wenzangu Okwi na Kazimoto na wengine waliondoka, lakini mimi nimeendelea kuwapo,” alisema Mkude.

Mkude ni miongoni mwa wachezaji waliochangia kwa kiasi kikubwa ubingwa wa Simba kama ilivyo kwa Okwi aliyecheka na nyavu mara 20, huku Kazimoto akitoa mchango mdogo sana kutokana na kutopewa nafasi mara kwa mara.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU