MSIKIE GUARDIOLA ALICHOSEMA KUHUSU YAYA TOURE

MSIKIE GUARDIOLA ALICHOSEMA KUHUSU YAYA TOURE

5705
0
KUSHIRIKI

MANCHESTER, England


 

 

KOCHA wa klabu ya Manchester City amesema kuwa, anashangazwa na yanayosemwa kuwa alikosea kumuuza kiungo, Yaya Toure, alipokuwa akiinoa klabu ya Barcelona, kwani anaamini yalikuwa ni maamuzi sahihi, hasa kwa manufaa ya mchezaji mwenyewe.

Guardiola alisema hayo huku akigusia namna Toure alivyopata mafanikio mara tu alipotua Man City, akitokea Barcelona na kuongeza kwamba, haoni kama alifanya makosa kumwondoa kwenye kikosi chake.

Toure anatarajiwa kuondoka kwenye viunga vya Etihad mwishoni mwa msimu huu, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuvaa medali nyingine ya ubingwa wa Ligi Kuu England, akiwa na matajiri hao wa Manchester.

Guardiola alithibitisha wiki iliyopita kuwa Toure hatasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

“Siwezi kukataa moja kwa moja kwamba nilifanya kosa kumuuza Yaya, nani ambaye hafahamu ubora wake? Labda nilifanya kosa kweli,” alisema kocha huyo.

“Lakini upo wakati inabidi yafanyike maamuzi na yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Lakini mimi naamini ni maamuzi mazuri na nilimtakia kila la heri. Nafahamu wazi jinsi alivyoishi kwa furaha hapa (Man City). Amepata mafanikio makubwa na anapendwa na wote. Nina matumaini ataagwa vizuri,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU