NEYMAR AOMBA MASHABIKI MARSEILLE WAADHIBIWE

NEYMAR AOMBA MASHABIKI MARSEILLE WAADHIBIWE

1064
0
KUSHIRIKI

PARIS, Ufaransa

NEYMAR amewataka mabosi wa mamlaka za soka hapa Ufaransa kuwashughulikia mashabiki wa Marseille kwa kitendo chao cha kumrushia vitu akiwa uwanjani.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita wakati PSG ikipata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo wa ugenini.

Mabao ya Kylian Mbappe na Julian Draxler, yaliihakikishia PSG pointi tatu ukiwa ni ushindi wao wa 11 mfululizo tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligue 1.

“Halikuwa jambo zuri kabisa. Nafikiri mamlaka, si tu mwamuzi, zinatakiwa kuchukua hatua,” alisema Mbrazil huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU