NYOSSO ATAKIWA YANGA KWA KAZI MAALUMU

NYOSSO ATAKIWA YANGA KWA KAZI MAALUMU

7311
0
KUSHIRIKI

NA HUSSEIN OMAR


Atamba akitua Jangwani timu hiyo haitachezewa na ‘vivulana’

BEKI wa kati wa Kagera Sugar, Juma Nyosso, amesema yuko tayari kutua Yanga endapo mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara wataweka mezani mzigo wa kutosha.

Akizungumza na BINGWA juzi, Nyosso alisema hana tatizo kujiunga na Wanajangwani hao, endapo watamhitaji kuboresha kikosi chao msimu ujao.

“Mimi sina tatizo, mpira ni kazi yangu. Hizo habari za kutakiwa na Yanga nimezisikia, lakini kama kweli wana nia, waje tuzungumze, nikawafanyie kazi na kurejesha heshima katika safu yao ya ulinzi na klabu kwa ujumla,” alisema Nyosso.

Nyosso alisema akiikosa Yanga, yupo tayari kuitumikia timu yoyote, kwani bado ana uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara na hata michuano ya kimataifa.

Safu ya ulinzi ya Yanga msimu huu imekuwa si ya kutisha sana kiasi cha ‘kuzoewa’ na hata wachezaji chipukizi waliowaliza, wakiwamo Yahya Zayd na Shaaban Iddi Chilunda wa Azam, Idd Seleman ‘Ronaldo’ wa Mbeya City na wengineo.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya wiki mbili baada ya kutolewa katika michuano ya SportPesa Super Cup inayoendelea mjini Nakuru, Kenya.

Yanga ilitolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 3-1 na Kakamega FC na hivyo kuendeleza gundu lao lililoanzia Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushindwa kutetea ubingwa wao walioporwa na watani wao wa jadi, Simba………

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA hapo juu

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU