PLUIJM AMTAKA CHIRWA AZAM

PLUIJM AMTAKA CHIRWA AZAM

2579
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU

KOCHA wa Singida United, Hans van dee Pluijm, inadaiwa ameutaka uongozi wa kikosi hicho kumnyakua mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa ili afanye naye kazi katika kikosi hicho cha matajiri hao wa Bongo.

Chirwa ambaye amekuwa katika kiwango kizuri ndani ya kikosi chake ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ni kati ya washambuliaji tishio kwa sasa.

Habari za uhakika zilizolifikia BINGWA jana, zimesema kuwa, baada ya mazungumzo na viongozi wa Azam, Pluijm aliweka pendekezo la Chirwa kujiunga na timu hiyo.

“Pluijm ameomba aje na Chirwa Azam, ili kuongeza nguvu katika kikosi chao, lazima atatia presha katika timu hii ambayo haieleweki msimu huu kwenye mbio za ubingwa,” kilisema chanzo chetu cha uhakika.

Pluijm anatarajia kurithi mikoba ya Aristica Cioiba, ambaye amepata timu nchini Abu Dhabi.

Lakini mpaka anakubaliana na Azam, Pluijm alikuwa ameichomolea timu yake ya zamani ya Yanga, akiwaeleza wazi kuwa hawezi kurudi kuifundisha timu hiyo kwani ana mapenzi ya kufundisha Azam.

Juzi, Yanga walikaa na kocha huyo Mholanzi, kumtaka arudi kuokoa jahazi katika kipindi hiki kigumu ambacho kocha wao, Mzambia George Lwandamina ametimkia kwao Zambia na kujiunga na klabu yake ya zamani Zesco United, kwa kile kinachodaiwa amekimbizwa na ukata jangwani.

Pluijm ni miongoni mwa makocha wenye heshima kubwa hapa nchini, akiwa ameiongoza vema Yanga kwa vipindi viwili tofauti, akiipa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara.

KUSHIRIKI
Makala ya awaliDJUMA HUYOO YANGA
Makala ijayoBADO WAO

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU