RAPHAEL DAUD ATEMA CHECHE

RAPHAEL DAUD ATEMA CHECHE

6153
0
KUSHIRIKI

MARTIN MAZUGWA


 

KIUNGO mpya wa klabu ya Yanga, Raphael Daud, amesema anaamini watafanya vizuri katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sport, mtanange unaotarajiwa kupigwa Mei 16, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ugenini dhidi ya USM Alger ya Algeria, walipokubali kichapo cha mabao 4-0.

Akizungumza na BINGWA, Daudi alisema mapumziko waliyoyapata tangu walipocheza dhidi ya USM Alger, yamewasaidia na anaamini wataingia katika mchezo huo wakiwa na nguvu mpya ya kuipigania timu hiyo.

“Yanga ni timu kubwa, tupo katika kipindi cha mpito hivi sasa, tutafanya vizuri katika mchezo ujao ili tuweke mazingira mazuri katika kundi letu,” alisema.

Daudi alisema    mashabiki wanapaswa kuwapa sapoti zaidi katika kipindi hiki ambacho watakuwa wakiliwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa.

Kiungo huyo ambaye amekuwa katika kiwango bora hivi sasa, amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mbeya City ya jijini Mbeya, hii ni mara yake ya kwanza kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU