ROBBEN AKIRI NJIAPANDA BAYERN

ROBBEN AKIRI NJIAPANDA BAYERN

5880
0
KUSHIRIKI
DORTMUND, GERMANY - MARCH 05: Arjen Robben of Bayern Munich runs with the ball during the Bundesliga match between Borussia Dortmund and FC Bayern Muenchen at Signal Iduna Park on March 5, 2016 in Dortmund, Germany.bs (Photo by Boris Streubel/Getty Images)

MUNICH, Ujerumani

WINGA Arjen Robben, ameweka wazi kuwa haelewi hatima yake klabuni hapo, hivyo ni ngumu kuthibitisha kama atabaki au atafungasha virago vyake.

Licha ya kwamba ni mmoja kati ya wachezaji muhimu Bayern, Robben hajapewa mkataba mpya, huku ikielezwa kuwa mabosi wa timu hiyo, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni umri wake wa miaka 34.

Kama ilivyo kwa Franck Ribery, Robben atamaliza mkataba wake wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Kwa upande mwingine, bosi wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge, alisema hatima ya wawili hao itafikia tamati wiki za awali za mwezi ujao.

Lakini, inasemekana kuwa Robben hafurahishwi na kitendo cha mazungumzo ya mkataba wake mpya kuchukua muda mrefu.

Wakati hali ikiwa hivyo, Bayern wanajiwinda na mchezo wao wa kesho dhidi ya Borussia Dortmund kabla ya kuwafuata Sevilla Machi 3, mwaka huu, katika mtanange wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU