RONALDO ANENA KUHUSU URENO

RONALDO ANENA KUHUSU URENO

5746
0
KUSHIRIKI

LISBON, Ureno


NYOTA wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi kuwa, kikosi hicho hakitaweza kufanya maajabu ya kuubeba ubingwa wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu nchini Urusi.

Mabigwa hao wa fainali za Euro za mwaka juzi, watafungua pazia la hatua ya makundi dhidi ya Hispania, mchezo wa Kundi B utakaochezwa Juni 15.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ronaldo alisema: “Ninachoweza kusema ni tamaa ambayo tunayo wachezaji na benchi la ufundi.

“Tunajua hatuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri, lakini tutafanya kama ilivyokuwa katika fainali za Euro mwaka juzi, lolote linaweza kutokea,” aliongeza.

Ronaldo ni tegemeo na nahodha katika kikosi cha Ureno na katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa na mafanikio makubwa akiwa na klabu anayoichezea ya Real Madrid.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU