SAFU YA USHAMBULIAJI YAMSIKITISHA WENGER

SAFU YA USHAMBULIAJI YAMSIKITISHA WENGER

488
0
KUSHIRIKI
LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema kwamba, tatizo la safu yake ya ushambuliaji kukosa makali ndilo jambo kubwa linalomsikitisha.

Juzi Gunners ikiwa haina nyota wake, Alexis Sanchez na Mesut Ozil, ilijikuta ikichapwa kwa mabao 2-1 na  Bournemouth wakiwa ugenini  katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Vitality, staa aliyesajiliwa kwa bei mbaya, Alexandre Lacazette  na mwenzake, Danny Welbeck, walishindwa kuziona nyavu na hivyo kumfanya Wenger aanze kukuna kichwa ili kutafuta mbadala  wa  Sanchez ambaye huenda akaenda Manchester City ama Manchester United.

“Sisononeshwi na morali wa timu,” alisema Mfaransa huyo.

“Ila kinachonisononesha zaidi ni tatizo la kutokuwa tishio kiasi cha kutosha. Tunakosa makali dakika za mwisho,” aliongeza Wenger.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU