SAMATTA ATUA ROMANIA

SAMATTA ATUA ROMANIA

1577
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU,

MTANZANIA Mbwana Samatta anazidi kupasua mawimbi ya anga za kimataifa kwani leo hii yuko nchini Romania na kikosi chake cha Genk ya Ubelgiji, ambapo watashuka uwanjani kucheza na Astra michuano ya UEFA ndogo.

Kikosi hicho cha akina Samatta kimefika hatua hiyo, baada ya kuongoza Kundi lao F wakiwa na pointi 12, mbele ya Athletic Club ya nchini Hispania waliomaliza na pointi 10 ambapo timu hizo mbili ndizo zilizofanikiwa kuvuka kwenye kundi hilo.

Timu nyingine zilizokuwa kwenye kundi hilo lakini pointi zao hazikutosha kuwavusha ukiachilia Genk na Athletic Club, ni Rapid Wien ya nchini Austria iliyomaliza ikiwa na pointi sita nafasi ya tatu na Sassuolo iliyomaliza mkiani na pointi zao tano.

Kama Genk itafanikiwa kuwaondosha wapinzani wao hao kwenye michuano hiyo, inaweza ikapangwa na timu vigogo wakiwamo Manchester United na kuwa fursa kwa Samatta kukabiliana na akina Paul Pogba.

Samatta alisajiliwa na Genk msimu uliopita baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiiwezesha TP Mazembe ya Congo, kutwaa ubingwa wa Afrika kwa upande wa klabu huku yeye akiibuka mchezaji bora kwa wale wanaocheza ndani ya Bara la Afrika.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU