Shilole atamani Rostam arudi Igunga

Shilole atamani Rostam arudi Igunga

2579
0
KUSHIRIKI

NA KYALAA SEHEYE

STAA wa muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amesema anatamani mfanyabiashara Rostam Azizi arudi katika nafasi ya ubunge kwenye Jimbo la Igunga ili na yeye ahamishie biashara zake mkoani Tabora, kwani kutakuwa na fursa nyingi.

Akizungumza hivi karibuni, Shilole alisema wakati Rostam alipokuwa mbunge wa jimbo hilo, hakuwahi kufikiria kuishi Dar es Salaam, kwa sababu kulikuwa na fursa nyingi za kibiashara tofauti na alipoachia ngazi.

“Niseme kutoka moyoni, Dar tayari nimewekeza vitu vingi, ikiwemo kujenga nyumba yangu, ila Rostam Azizi akirudi tu Igunga basi huku nitatafuta usimamizi, nitarudi Igunga kuwekeza tena kwa kuwa nina imani uchumi wa eneo lile utapanda kwa kasi na inaweza kuwa kituo cha pili kibiashara ukiacha Dar es Salaam,” alisema Shilole.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU