SIMBA YA MSIMU UJAO WATAPATA TABU SANA

SIMBA YA MSIMU UJAO WATAPATA TABU SANA

3261
0
KUSHIRIKI

NA ALLY KAMWE, KENYA


WAPINZANI wa Simba msimu ujao huenda wakapata tabu sana kutokana na makocha wa timu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi, kutoridhishwa na idadi ya mabao yaliyofungwa na washambuliaji wao msimu uliomalizika.

Simba wamefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika hivi karibuni, wakibeba ubingwa kwa kukusanya pointi 69 na kufunga jumla ya mabao 62.

Kati ya hayo 62, mabao 34 yamefungwa na washambuliaji wao wawili ambao walikuwa wakiwategemea zaidi, Emmanuel Okwi aliyetikisa nyavu mara 20 na nahodha John Bocco akitupia 14.

Kitendo hicho cha kuwategemea washambuliaji wawili pekee kimelifanya benchi la ufundi la timu hiyo, linaloongozwa na kocha Pierre Lechantre na msaidizi wake, Masoud Djuma, kuhitaji kuongeza washambuliaji watatu wa kigeni.

Akizungumza na BINGWA jana nchini Kenya, kocha msaidizi, Masoud Djuma, alisema wanaiangalia zaidi safu ya ushambuliaji kwa sababu msimu ulioisha waliteseka  kutokana na kuwategemea washambuliaji wawili, Okwi na Bocco.

 

“Msimu uliopita tuliteseka sana kwa kuwategemea Okwi na Bocco pekee, hilo hatutaki tena litokee msimu ujao, ndio maana unaona tumeanza kusajili washambuliaji, tunataka kufunga mabao mengi kwenye kila mechi,” alisema Djuma.

Akiongeza kile alichokisema msaidizi wake, Pierre, alidai malengo yao ya…….

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA hapo juu

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU