SIRI YA KIPAJI CHA KANTE YAGUNDULIKA

SIRI YA KIPAJI CHA KANTE YAGUNDULIKA

693
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

MKURUGENZI wa soka wa klabu ya Everton, Steve Walsh ambaye alimwibua kiungo mkabaji wa Chelsea, N’Golo Kante, amefafanua hatua alizozitumia kuibua vipaji na kujizolea umaarufu alipokuwa kwenye klabu ya Leicester City misimu kadhaa iliyopita hadi timu hiyo iliponyakua ubingwa wa Ligi Kuu England.

Walsh alinyakuliwa na Everton majira yaliyopita ya kiangazi, baada ya mabosi wa klabu hiyo kuridhishwa na rekodi yake ya kugundua vipaji na kuvileta Leicester, wakiwamo Kante, Jamie Vardy na Riyad Mahrez.

“Jambo la muhimu ni utayari wa wachezaji, hauwezi kujiridhisha kwa kuangalia nini wanachokifanya wakiwa na mpira lakini umegundua utayari wao wa kuutafuta mpira pindi wanapoukosa? Je, wako tayari kujituma ili kuisaidia timu kwenye hali yoyote mchezoni? Wanafahamu namna ya kujipanga kiulinzi kama wanavyoshambulia?

“Ukishawapata, sasa hakikisha unazungumza na kule ulipowatoa, pia zungumza nao kuhusu namna gani alivyokuwa akiishi kule. Hapo utakuwa umekamilisha kazi yako na ni lazima utampata mchezaji sahihi,” alisema.

Kante ameibuka kuwa mchezaji bora aliyeibuliwa hivi karibuni, akiisaidia Leicester kunyakua ubingwa wa ligi kuu na tangu alivyoondoka na kutua Chelsea, pengo lake halijaweza kuzibika pale Leicester.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU