STAND UNITED WAMFUNGIA KAZI MAKAMBO

STAND UNITED WAMFUNGIA KAZI MAKAMBO

4509
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI


TIMU ya Stand United imemfungia kazi mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo, huku wakimwambia  asitarajie mteremko kwani hatapata nafasi ya kuwafunga watakapokutana  Septemba 16, mwaka huu.

Stand United ambayo kwa sasa imeweka kambi Kahama, inatarajia kucheza  na Yanga mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal, alisema safu yao ya ulinzi ipo vizuri na hakuna straika wa Yanga anayewapa presha.

Alisema kabla ya mechi hiyo watacheza mechi za kirafiki na Jumamosi wanatarajia kucheza na Kahama Kombaini ili kuangalia kama eneo lao la ushambuliaji limekaa sawa baada ya kulifanyia kazi mazoezini.

“Yanga hivi sasa ni timu ya kawaida, hakuna  cha kuhofia kukutana nayo,  huyo mshambuliaji wao (Makambo) tunamsikia lakini sidhani kama kwetu itakuwa rahisi kupenya, tumejiandaa na tunaendelea kujipanga,” alisema Bilal.

Alifafanua kuwa wanashukuru wameanza msimu vizuri, wakicheza mechi tatu na kupoteza mmoja pekee, hivyo wanataka kuendelea kupambana  ili wasirudi nyuma.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU