SUAREZ- BARCA IMETOLEWA? TULIENI VITA BADO MBICHI

SUAREZ- BARCA IMETOLEWA? TULIENI VITA BADO MBICHI

649
0
KUSHIRIKI

CATALONIA, Hispania

STRAIKA wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez, amesema bado wana matumaini ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kichapo cha mbwa mwizi walichokipata kutoka kwa PSG wiki iliyopita.

Mabingwa hao watetezi wa La Liga walinyukwa mabao 4-0 na PSG kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliopigwa nchini Ufaransa.

Kutokana na kichapo hicho, Barca wanakabiliwa na jukumu la kushinda mabao kuanzia 4-0 katika mchezo wa marudiano utakaopigwa katika dimba la Nou Camp Machi 8, lakini historia ya michuano hiyo inasema haijawahi kutokea timu iliyobamizwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano na kusonga mbele.

“Kama tunataka kujenga historia ndani ya klabu hii, ni lazima tugeuze haya matokeo. Sisi ni timu bora duniani, tunao uwezo wa kugeuza matokeo haya kwenye nyakati ngumu kama hizi,” alisema Suarez.

Barcelona imenyakua taji la Ulaya au Ligi ya Mabingwa mara tano na katika miaka tisa mfululizo ya hivi karibuni imeweza kutinga robo fainali.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU