TAMBWE: OKWI ATAFIKIA REKODI YANGU

TAMBWE: OKWI ATAFIKIA REKODI YANGU

5163
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

KASI ya upachikaji mabao aliyonayo straika  wa Simba, Emmanuel Okwi, inaonekana kumshtua mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, ambaye amesema hatashangaa kuona Mganda huyo anaifikia rekodi yake aliyoiweka msimu wa 2015/16.

Katika msimu huu, Okwi ameshacheka na nyavu mara 17 hadi sasa ikiwa pungufu ya mabao manne aliyoyafunga Tambwe katika msimu wa 2015/16 na kuibuka mfungaji bora.

Tambwe aliliambia BINGWA kuwa, yeye aliweza kufunga idadi hiyo ya mabao baada ya kumalizika kwa michezo 26 ya Ligi Kuu, lakini Okwi ameshafunga 17 katika mechi 22 huku zikiwa zimebaki nane.

“Kama hatakuwa na tatizo litakalomweka nje ya uwanja mabao manne yaliyobaki si mengi kwa michezo minane iliyobaki, hivyo bila shaka ana nafasi kubwa ya kuvunja rekodi yangu.

“Mchezaji mwenzako anapofanya kazi nzuri si jambo baya kumpongeza, binafsi nampa pongezi nyingi Okwi kwa kile anachokifanya tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kipindi anasajiliwa,” alisema Tambwe.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU