TIBER JOHN ALITAMANI KUWA MNENGUAJI

TIBER JOHN ALITAMANI KUWA MNENGUAJI

5204
0
KUSHIRIKI

NA GLORY MLAY

HATIMAYE mshambuliaji, Tiber John, amejiunga na Singida United na kuzitosa Simba, Yanga na Azam FC ambazo zilikuwa zikimfukuzia kwa udi na uvumba.

Nyota huyo ambaye msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara amekipiga Ndanda FC na kufunga mabao manne, akitoa ‘assist’ sita, ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha.

Kutokana na uwezo wake wa kuchezea mpira, wachezaji wenzake wa Ndanda FC wamempachika jina la Neymar Mweusi.

Je, ulishawahi kujiuliza kama si soka Tiber angekuwa anafanya kazi gani?

Akizungumza na BINGWA juzi, Tiber alisema kuwa kama si soka angekuwa mnenguaji ‘dancer’ kwani ni kazi ambayo alikuwa anaipenda.

“Kazi ya unenguaji ni nzuri kwa sababu inakupatia fedha kwa haraka, pia ni kitu ambacho ninakipenda kutoka moyoni na sifanyi kisa fulani kafanya hapana, ni mapenzi yangu ndiyo yalinituma kupenda kazi hiyo,” anasema Tiber.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU