TIMU ALI KIBA YAKOSA UWANJA WA MAZOEZI

TIMU ALI KIBA YAKOSA UWANJA WA MAZOEZI

6694
0
KUSHIRIKI

NA JEREMIA ERNEST


STAA wa Bongo Fleva, Ali Kiba, amesema mpaka sasa timu yake haijapata uwanja wa mazoezi, licha ya kubaki siku moja kuelekea mchezo wa kuchangia ujenzi wa shule za msingi dhidi ya timu Mbwana Samatta.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Taifa jana, Ali Kiba alisema programu ya NIFUATE ambayo inaendesha mchezo huo, utakaopigwa katika dimba la Taifa kesho, itakuwa endelevu, huku mapato yakienda kusaidia shule za msingi, kwani ndiyo msingi wa elimu.

“Mpaka sasa bado hatujapata uwanja wa mazoezi na kocha wetu tunatarajia awe Julio Kihwelo, tukipata uwanja tutatangaza kupitia mitandao ya kijamii, michezo ni afya  na burudani pia, nitaanza kusaidia shule yangu niliyosoma ya Upanga,” alisema Kiba.

Katika hatua nyingine, Kiba alisema sababu ya kutoweka picha ya Sam wa Ukweli katika ukurasa wake wa picha ni kutokana na dini yake kukataza, lakini wataonyesha kuguswa siku ya mchezo huo kwa kuvaa vitambaa vyeusi katika mkono.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU