TUZO YAMTOA POVU RIYAMA

TUZO YAMTOA POVU RIYAMA

6945
0
KUSHIRIKI

NA JEREMIA ERNEST

NYOTA wa filamu nchini, Riyama Ally amesema hakuwa na taarifa za jina lake kuingizwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Sinema Zetu zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Riyama Ally ambaye alikuwa kwenye kipengele cha Mwigizaji Bora wa Kike kupitia filamu Mama wa Marehemu, ameliambia Papaso la Burudani kuwa waandaaji wa tuzo hawakumpa taarifa hivyo alishindwa kuomba kura kwa mashabiki zake.

“Sikupata taarifa yoyote kama nimeingia kwenye kinyang’anyiro ila wiki moja kabla prodyuza wa filamu ya Mama wa Marehemu, alinijulisha kuwa kuwa ametumwa anifishie ujumbe kuwa nipo kwenye tuzo, nikapewa na kadi za mwaliko ila niliziacha sababu nilikuwa sijajiandaa kwa lolote,” alisema Riyama ambaye aliwahi kushinda tuzo ya Miwgizaji Bora wa Kike mwaka 2005.

Papaso la Burudani lilimtafuta Msemaji wa tuzo hizo Mariam Mohammed ambaye alisema wao hawakuchagua filamu bali waliletewa filamu na wamiliki.

“Wamiliki walileta filamu, aliyeleta filamu hiyo alipaswa kuwafahamisha wahusika walioshiriki katika filamu yake,” alisema Mariam.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU