WAZIRI MKUU KUFUNGUA UMISSETA MWANZA LEO

WAZIRI MKUU KUFUNGUA UMISSETA MWANZA LEO

3322
0
KUSHIRIKI

NA GLORY MLAY


 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi ya mashindano ya  Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari (Umisseta), ngazi ya Taifa yanayoanza leo hadi Juni 15, mwaka huu jijini Mwanza.

Mashindano ya mwaka huu ni ya saba kufanyika kitaifa, baada ya kuanzishwa tena tangu yalipositishwa mwaka 2000, ambapo yatafanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza.

Wanamichezo 3,360 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo wakitokea mikoa 28 upande wa Umisseta, ambapo 26 ni kutoka Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar.

Kwa upande wa michezo ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Msingi (Umitashumta), itakayoanza Juni 17, mwaka huu na mikoa itakayoshiriki ni 26 kutoka Tanzania Bara pekee.

Katika Umisseta michezo itakayochezwa ni soka, mpira wa wavu, mikono, kikapu, meza na riadha kwa jinsia zote, pete kwa wasichana, bao kwa wavulana, riadha maalumu kwa wenye ulemavu, sanaa za maonyesho ikiwamo kwaya, ngoma, ngonjera na mashairi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Tamisemi, Selemani Jafo, imewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa mkoa yao inapeleka wachezaji wanafunzi tu na si vinginevyo.

Taarifa hiyo pia imewataka waamuzi kuchezesha kwa kuzingatia kanuni na sheria bila kuwepo upendeleo ili washindi wa michezo yote wapatikane kwa haki.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU