WEMA SEPETU APATA DILI AFRIKA KUSINI

WEMA SEPETU APATA DILI AFRIKA KUSINI

7882
0
KUSHIRIKI

NA KYALAA SEHEYE

SIKU chache baada ya kutwaa tuzo mbili katika Tamasha la Kimataifa la Sinema Zetu (SZIFF), Malkia wa kiwanda cha filamu nchini Wema Sepetu, ameingia mkataba na kampuni ya Obuntu Africa yenye maskani yake Afrika Kusini.

Wema ameliambia Papaso la Burudani kuwa kampuni hiyo itaisambaza filamu yake ya Heaven Sent katika nchi saba za Afrika hivyo kuendelea kufanikiwa na kudhihirisha uhalali wa ushindi wake ambao umekuwa ukitiliwa shaka na baadhi ya wasanii wenzake wakike.

“Ninamshukuru sana Mungu hapa nilipofika na nimeanza kujua nini thamani yangu ndani ya tasnia ya filamu. Tuzo nilistahili ndiyo maana nimepewa mkataba huu mnono, ninachowaomba na wao wajitahidi  kufaya kazi ambazo hakimiliki itakuwa mali yao ili waweze kushiriki mwakani,” alisema Wema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU