WENGER ATAMANI KUIONGOZA PSG

WENGER ATAMANI KUIONGOZA PSG

8248
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


 

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amegoma kuikataa ofa ya kuwa Meneja Mkuu wa PSG mara tu atakapoondoka Emirates mwishoni mwa msimu huu.

Wenger mwenye umri wa miaka 68, alinukuliwa mapema wiki hii kuwa ameshapata ofa nyingi zaidi ya alizotarajia tangu alipotangaza kuwa huu ndio msimu wake wa mwisho kama kocha wa ‘The Gunners’.

Mfaransa huyo alihusishwa kujiunga na PSG, aidha awe mrithi wa kocha mkuu wa sasa, Unai Emery au kuchukua majukumu mengine ya uongozi iwapo mabingwa hao wa Ligue 1 wangemwajiri Thomas Tuchel kuwa kocha wao.

Licha ya kwamba Wenger anavutiwa kuendelea na kazi ya ukocha, pia hakukataa mabadiliko iwapo atapewa majukumu mengine.

“Nitaamua pia kama nitachukua jukumu la kuwa Meneja Mkuu, nahitaji nibadilike ingawa bado sijaamua, ninaweza kusema ndio nitaendelea na ukocha lakini baadaye nitabadilika na kusema ngoja nifanye mengine, ila kwa sasa sina jibu kamili,” alisema.

Wenger pia anahusishwa kunyakuliwa na Napoli, iwapo klabu hiyo ya Italia itampoteza kocha wao wa sasa, Maurizio Sarri anayetajwa kutakiwa na Chelsea.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU