YOUNG KILLER, KHALIGRAPH JONES KUONYESHANA UWEZO KESHO

YOUNG KILLER, KHALIGRAPH JONES KUONYESHANA UWEZO KESHO

4391
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KATIKA kusherehekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa msanii wa hip hop, Erick Msodoki ‘Young Killer’, msanii huyo amemdondosha nchini rapa kutoka Kenya, Khaligraph Jones, tayari kwa kukonga nyoyo za mashabiki zao kesho ndani ya Ukumbi wa Club Next Door, Masaki, Dar es Salaam.

Young Killer ameliambia Papaso la Burudani kuwa, toka rapa huyo ameshirikishe kwenye wimbo wa How We Do, hawajawahi kutumbuiza pamoja, hivyo siku hiyo ni muhimu kwao kuwapa burudani mashabiki kwa kuonyeshana uwezo.

“Kutakuwa na wasanii wengi kutoka hapa Bongo ila mgeni wangu ni Khalighaph, tutakata keki pamoja na kuwaonyesha mashabiki kile tulichonacho,” alisema Young Killer

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU