Monday, August 10, 2020

Amri Said angetumia busara kwa kipa wake

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA WINFRIDA MTOI

BAADA ya mechi ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Yanga na Biashara United, kitu kilichozua gumzo kubwa ni kitendo cha Kocha wa Biashara, Amri Said, kuonekana akirushiana maneno na mlinda mlango wake, Nurdin Balora, baada ya kumfanyia mabadiliko.

Mlinda mlango huyo alipofika katika benchi baada ya kupumzishwa alionekana kuanza kurushiana maneno na Amri, ambaye aliamua kumwita mwamuzi Martin Sanya amtoe nje kabisa, hivyo Balora aliondolewa kwenye benchi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo, Amri alisema Balora ni mlinda mlango wa kawaida na alikuwa na uwezo wa kumtoa nje muda wowote na hata kumfukuza kabisa katika timu yake, kwa sababu anahitaji wachezaji wenye nidhamu.

Majibu ya kocha huyo yalishtua na kuonyesha wazi kuna tatizo kati ya wawili hao kabla ya mchezo huo kutokana na jinsi alivyoonekana akijibizana naye.

Kuna siku moja Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ambaye ni mmoja wa watu wanaosimamia nidhamu katika kikosi chake na hapendi mchezaji yeyote awe juu ya wengine, alisema kuwa mchezaji wake anapofanya makosa uwanjani anamsubiri mazoezini ndipo atamsema.

Zahera alisema siku moja au mbili baada ya mechi ndipo hukaa na wachezaji wake na kuwasema juu ya makosa wanayofanya na kutozingatia maelekezo yake, wakiwa hawana presha yoyote.

Alisema kwa kawaida kocha hutakiwi kuzungumza na mchezaji kitu kibaya kwake muda mfupi baada ya mechi kwasababu anaweza kukujibu vibaya ukakasirika kutokana na presha aliyotoka nayo uwanjani.

Hata kwa Amri, licha ya kukasirishwa na kipa wake, hakutakiwa kurushiana maneno na mchezaji mbele ya mashabiki na wachezaji wenzake, kwani inaleta picha mbaya na kuonyesha wazi jinsi mnavyoishi vibaya.

Pia kitendo kile cha kutoa maneno makali kwa mchezaji mbele ya wenzake kinawapotezea morali wengine na kuwafanya wawe na hofu pindi wanapopewa nafasi ya kucheza kwa kipindi kile.

Ni kitendo ambacho hakikuwa cha kiungwana kwa kocha mwenye jina kubwa na aliyewahi kucheza soka kwa muda mrefu na anafahamu makosa ya uwanjani na kuamua kufokeana na mchezaji.

Lakini kwa mtazamo wangu, hata kama kipa alikuwa na makosa, Amri atatupiwa lawama kwa kilichotokea kwa sababu yeye alisimama katika benchi la ufundi akiwa ni kiongozi.

Kuna misemo mingi inaelezea namna kiongozi atavyotakiwa kuwa, ambapo wapo wanaosema uongozi ni sayansi ambayo inakuwa na mambo mengi, hivyo ukiwa katika nafasi hiyo lazima kuepuka mambo yanayoweza kukuharibia sifa.

Kiongozi anatakiwa kuwa wa mfano katika uvumilivu wa changamoto, kwa sababu utakumbana na mambo mengi ya kukukatisha tamaa au kukuharibia usiweze kufikia malengo ya kile unachohitaji.

Hali ya kuonyesha jazba, hasira mbele za watu kwa wale unaowaongoza ni udhaifu, kwani zipo njia nyingine za kutumia ili kuondoa changamoto fulani.

Ikumbukwe pia Amri ni mwalimu aliyepitia mafunzo ya ukocha, yupo Biashara United si kwa uzoefu pekee, bali kwa taaluma ya soka aliyonayo ambayo inabeba vitu vingi vinavyosaidia kujua ni jinsi gani ya kuishi na wachezaji ambao kila mmoja ana malezi yake.

Miongoni mwa vitu ambavyo makocha wanafundishwa katika kozi zao ni saikolojia, hii inamsaidia kukabiliana na changamoto za kibinadamu kwa sababu inajulikana wachezaji ni kama wanafunzi, kujua tabia ya kila mmoja ni muhimu.

Ukiachana na mafunzo ya ukocha, pia uzoefu wa kucheza soka kwa Amri Saidi, ni wazi anafahamu tabia za wachezaji na hali wanayokuwa nayo pindi wanapotoka uwanjani kulingana na mchezo ulivyokuwa.

Ukiangalia mchezo wa juzi, ilikuwa ni lazima mmoja atoke na mwingine kusonga mbele, hivyo matokeo yalivyokuwa kila mchezaji hakuwa katika hali nzuri, walifikiria zaidi nini kitatokea endapo watatupwa nje ya michuano hiyo.

Si rahisi kwa mtu kukuelewa wakati ule mechi inaendelea kama ilishindikana kumrekebisha katika mazoezi, ni dhahiri pale mngeishia kutupiana maneno, kwa kuwa kila mmoja alikuwa na presha.

Migogoro ni jambo la kawaida watu wanapoishi pamoja, lakini kiongozi anatakiwa kuwa na busara zaidi kuepusha kuharibu malengo, ili timu ifanye vizuri kocha ni mtu wa kwanza anayetakiwa kuzuia hasira zake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -