Sunday, January 17, 2021

Lwandamina, ishi vizuri na Niyonzima uifurahie Yanga

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MWANDISHI WETU

MAISHA ya soka ni kama shuleni tu, kuna mwalimu na mwanafunzi, hapo utajua nani anatakiwa kumsikiliza mwenzake.

Lakini bado shule hiyo hiyo, atakuwepo tu mwanafunzi ambaye walimu wanamheshimu na anaweza kukaa nao meza moja wakazungumza. Ndio, anakuwa mwanafunzi msikivu mwenye kutekeleza maagizo lakini kwa wakati huo huo, hakuna atakayeweza kumtisha kwa njia yoyote.

Barcelona kuna mwanafunzi mtiifu wa La Masia, Lionel Messi. Huyu ametimiza yote aliyoagizwa pale Camp Nou lakini anaihitaji sana heshima kutoka kwa walimu wake, heshima inayompa furaha na hakuna atakayethubutu kumkera kwani kibarua chake kuota nyasi ni rahisi sana.

Tatizo lililokuja kumkuta mwalimu wake, Luis Enrique, ni kwamba hakujua kwamba Messi anapenda kuheshimiwa tangu alipoanza kusakata soka na timu ya wakubwa enzi hizo akiwa sambamba na watu kama Ronaldinho Guacho na wengineo.

Wakatalunya wanamtambua kama mfalme wao, ni kama walipunjwa uwepo wa jina lake kama mzaliwa wa Catalonia na si Rasario kule Argentina.

Enrique alipata shida sana jamani, kuanza kumtumia Messi kwenye nafasi anazozijua mwenyewe ni kosa kubwa alilotaka kulizoea katika nyakati zake za mwanzo kabisa kama kocha wa Barcelona na Messi hakuvutiwa na hili.

Messi, ama La Pulga kama wanavyomwita, alichukua uamuzi mmoja tu wa kuwauliza viongozi wa Barca, wanamtaka yeye au Enrique?

Naam, ni kiongozi gani ambaye angetaka kuziba masikio yake kumchunia Messi? Wote walikaa meza moja na Enrique na kumwambia ukweli: “Baba, huyu ni mwanetu sote, mlee kwa upole na unyeyekevu.”

Utakuwa ni mwanadamu mwenye roho ngumu kama utaamua kuwa mbishi kwa maneno ya vigogo wanaomnyenyekea Messi.

Messi anaweza kuwa si mwongeaji sana lakini akitoa neno pale Barcelona wanamsikiliza na wanatii, Enrique alitakiwa kuishi ndani ya neno-sheria la King Leo.

Wamekuja mastaa wangapi pale Barca na bado mfalme amebaki kuwa mfalme? Zlatan Ibrahimovic mnayemwona ana maringo, alikoma kuringa pale Nou Camp.

Si hapo tu Barca, kuna mwingine yupo Real Madrid, Cristiano Ronaldo, huyu naye kama ukitaka kuwa na amani Santiago Bernabeu, lazima umsikilize anataka nini, Jose Mourinho alipomkorofisha tu milango ilifunguliwa kwake.

Mkongwe wa tasnia ya ukocha duniani, Carlo Ancelotti, alimheshimu Mreno huyu, hakutaka kupanga kikosi cha Real Madrid bila kumpa Ronaldo nafasi ya kwanza ya kusema anachokitaka ndani ya klabu.

Bernabeu inaibeba Madrid, halafu inambeba mtoto wao Ronaldo.

Kwa nyakati tofauti, Barcelona na Real Madrid wamewahi kujaribu kumaliza ufalme wa Messi na Ronaldo kwa kuwaleta Neymar na Gareth Bale, lakini unajua nini kimetokea? Imeshindikana!

Ni sawa tu na hapa Tanzania kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu Yanga walivyoshindwa kuuondoa ufalme wa Haruna Niyonzima. Walipojaribu tu, tena kupitia aliyekuwa Katibu mkuu wao, Dk. Jonas Tiboroha, matokeo yake katibu huyo akatimka na jamaa akabaki Jangwani.

Niyonzima ni mwanafunzi anayehitaji dekezo la kipekee pale Jangwani. Unazijua faida za yeye kudekezwa? Ni burudani murua anayowapa mashabiki iwe ni uwanja wa Taifa au uwanja wa Uhuru.

Ubora wa miguu ya Niyonzima awapo kwenye ubora wake ni kitu kinachohitaji utulivu wa akili kuanza kukielezea kwa sababu ni maneno machache lakini yanayoeleweka na si maneno mengi, kwani anachokifanya uwanjani kinafanya watu wabaki midomo wazi, wasiwe na la kusema.

Kuna wakati mashabiki wa Yanga hutamani aondoke wakiamini muda wake umekwisha Jangwani, lakini anapokosekana dimbani vilio husikika wakishindwa kujua nani aliye sahihi kwa kuanza yeye asipokuwepo.

Ni ukweli usiopingika, Niyonzima hana mbadala Yanga tangu walipomnyakua kutoka APR mwaka 2011.

Walitaka kuamini kwamba Thabani Kamusoko ana vitu zaidi ya Niyonzima, wakamwondoa kikosini, wakamrudisha na anadhihirisha kwamba yeye ni bidhaa adimu.

Benchi jipya la ufundi linalokuja chini ya George Lwandamina, lina jukumu la kuhakikisha wanaenda sambamba na kile Niyonzima akitakacho ili waepukane na zahama alizowahi kuwasababishia wengine.

Ni jambo moja tu wanaloweza kulifanya na lisiwaletee matatizo, watafute kifaa kingine cha maana kupunguza ufalme wa Niyonzima (kuuondoa ni kazi ngumu).

Hawana budi kufanya hivyo ili maisha yao yawe mazuri kama Enrique Camp Nou.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -