Wednesday, October 28, 2020

OFA YA ULIMWENGU NI KUFURU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MOHAMED KASSARA


OFA ambayo straika wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, amewekeza mezani na mabingwa wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya Al Ahly ya Misri ni kufuru.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo BINGWA imeipata na kuthibitishwa na Meneja wa staa huyo, Jamal Kisongo, inasema kuwa Al Ahly wameweka mezani ofa ya mshahara wa Dola 400,000 (sawa na Sh milioni 860) kwa ajili ya straika huyo wa zamani wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza na BINGWA jana, Kasongo alisema ofa hiyo inamaanisha kuwa kwa mwezi Ulimwengu atakuwa analipwa Dola 33,000 (sawa na Sh milioni 71.6) dau ambalo ni refu sana ikilinganishwa na wachezaji wengi wanaocheza ndani ya nchi.

Kisongo aliendelea kusema kuwa licha ya dau hilo kutamanisha, lakini wamelitolea nje kwa sababu ndoto zao ni kuhakikisha straika huyo mwenye miaka 23 anacheza nje ya bara la Afrika.

Alisema mbali na Al Ahly, Ulimwengu pia ana ofa kutoka Sudan, Afrika Kusini pamoja na nje bara la Afrika katika nchi za Urusi, Ubelgiji, Hispania, Qatar na China, ingawa hakutaja klabu gani zinamuwania.

Kisongo ambaye pia ni Meneja wa Mbwana Samatta, aliongeza kusema kuwa kuna timu moja ya Ligi Kuu Ubelgiji na nyingine Daraja la Kwanza England pia zinamhitaji kwenda kufanya majaribio, lakini wamekataa kwa sababu Ulimwengi si mchezaji wa majaribio.

Meneja huyo alisema kinachosababisha Ulimwengu kuchelewa kujiunga na timu hizo ni majeraha ya goti aliyoyapata katika  moja ya mechi za Kombe la Shirikisho Afrika wakati akiwa TP Mazembe kabla ya timu hiyo kuchukua ubingwa mwaka huu.

“Ulimwengu kwa sasa amepona na ameanza mazoezi ya utimamu wa mwili, lakini amepata mwaliko wa kwenda kufanya  mazoezi katika  klabu ya Mamelody Sundown inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini,” alisema Kisongo.

Ulimwengu  alitokea katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu  Copa Coca cola na baadaye kulelewa katika Kituo cha Tanzania Soccer Academy  (TSA) kilichokuwa chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kabla ya kwenda Sweden na kujiunga na TP Mazembe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -