Tuesday, October 27, 2020

MAOMBOLEZO YA CHAPECOENSE… INASISIMUA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MEDELLIN, Colombia

MAELFU ya mashabiki Atletico Nacional walijazana kwenye Uwanja wa Atanasio Girardot, ambao ulipangwa kuchezwa fainali ya Copa Sudamericana, kuomboleza vifo vya timu pinzani Chapecoense waliofariki kwa ajali ya ndege.

Ndege waliokuwa wanasafiria wachezaji wa Chapecoense kwenda mjini Medellin, ilianguka juzi Jumatatu na kuua watu 76.

Uwanja huo wa Atletico, Atanasio Girardot Sports Complex ambao hubeba mashabiki 45,000, ulijawa na watu waliofika kwa ajili ya kuomboleza, huku wengine wakibakia barabarani.

Jumatano alfajiri ndio siku iliyotarajiwa kuchezwa fainali ya kwanza ya Copa Sudamericana kati ya Chapecoense na Atletico Nacional, hivyo mashabiki walitumia nafasi hiyo kuomboleza.

Mishumaa iliwashwa na maombi kufanyika, huku waombolezaji wakiwa wamevaa jezi za Chapecoense, ambapo njiwa walirushwa hewani kuwakumbuka watu wote waliofariki kwenye ajali hiyo.

Maua na mataji yalinunuliwa pamoja na bendera za Brazil na Colombia.

Kwenye video mbalimbali zilionyesha mashabiki wakiwa wanaimba kwenye uwanja huo, naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Jose Serra, alitoa shukrani kwa watu wa Colombia kwa moyo wao wa upendo waliouonyesha.

Pamoja na mashabiki hao wa Atletico Nacional, nao mashabiki wa Chapecoense walifanya maombolezo kwenye uwanja wa timu hiyo, Arena Conde nchini Brazil.

Pia kwenye mechi zilizofanyika barani Ulaya, kama ile ya Kombe la Mfalme la Real Madrid dhidi ya Cultural Leonesa, Madrid walivaa jezi zilizoandikwa ‘Sisi wote ni wa Chapecoense’.

Mchezo wa Kombe la Ligi kati ya Arsenal na Southmpton ulianza kwa kusimama kimya dakika moja kutoa heshima za mwisho kwa wachezaji wa Chapecoense waliofariki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -